23
May

MKUTANO maalum wa siku mbili wa wadau wa kisukari duniani kufanyika jijini dar

tdaMshauri Mganga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Hosipitali ya Shree Hindu Mandal, ambaye pia ni Katibu wa kitengo cha Watafiti wa ugonjwa wa kisukari Afrika Mashariki (EADSG) Dkt. Kaushik Ramaiya alisema umuhimu wa mbinu ya Taifa dhidi ya vita ya ugonjwa wa kisukari ni nyenzo muhimu kwa Taifa hili. Kushoto ni Pro. Ayoub Magimba -Kutoka Wizara ya Afya Tanzania,Dkt. Steven Shongwe, WHO-AFRO na kulia ni&Dkt. Mr. Anders Dejgaard: Mkurenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kisukari Duniani (World Diabetes Foundation)

Mkutano huo utahusisha Viongozi wa Mfuko wa kusaidia wagonjwa wa Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani Ofisi za Mikoa kwa Afrika pamoja na Shirikisho la Kisukari duniani watakaokutana kujadili mambo mbali kuhusu namna ya kusaidia wagonjwa wa ishio na Kisukari.

Tarehe 17 na 18 March 2016 Dar es Salaam, TANZANIA

MKUTANO huo maalum wa siku mbili wa wadau wa kisukari duniani ambao utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

Mshauri Mganga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Hosipitali ya Shree Hindu Mandal, ambaye pia ni Katibu wa kitengo cha Watafiti wa ugonjwa wa kisukari Afrika Mashariki (EADSG) Dkt. Kaushik Ramaiya alisema umuhimu wa mbinu ya Taifa dhidi ya vita ya ugonjwa wa kisukari ni nyenzo muhimu kwa Taifa hili.

Akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Mkutano huo Dkt Kaushik alisema “Linapokuja suala la kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kisukari Mkutano kama huo unachukua nafasi kubwa kwa wagonjwa waishio na Kisukari,”

“Kwa kuimarisha kile ambacho tumejifunza, na kubadilishana mambo muhimu miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, tutakuwa na uwezo wa kuwezesha yatokanayo baada ya Kongamano la Kisayansi na utafiti katika kufikia malengo, Mpango wa WHO Global Action kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, unahitajika.”

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kisukari Duniani (Wolrd Diabetes Foundation) Dkt Anders Dejgaard alisema mkutano huo ni kama kichocheo cha mabadiliko. “Ngarama za Matibabu kwa Wagonjwa wa Kisukari ni kubwa, Mfuko wa kusaidia Wagonjwa wa Kisukari Duniani ulianzishwa mwaka 2002, kwa maono ya kusaidia watu wanaoishi na ugonjwa huo katika nchi zinazoendelea,” anasema Anders Dejgaard.

“Tumekuwa tukisaidia kuzuia ugonjwa wa kisukari na upatikanaji wa huduma kwa watu walioathirika na ugonjwa huo katika ukanda wa Afrika tangu kuanzishwa kwa Mfuko huu. Leo, zaidi ya muongo mmoja amepita na mipango yetu imeonyesha matunda makubwa, shukrani kwa juhudi za pamoja za mabingwa wa ndani ya Nchi husika, washirika wa ndani ni muhimu katika kufikisha msaada wa huduma. Pengine ushiriki wa Prof Ayoub Magimba, Wizara ya Afya, Tanzania anaweza kuzungumzia kuhusu maendeleo makubwa ya Tanzania ndani ya eneo la huduma ya kisukari ya zaidi ya miaka 10-15 iliyopita,” amesema Dkt Anders Dejgaard.“

Mikutano huo unalenga kutatua matatizo yanayoambatana na Kisukari unalooendela kukua barani Afrika kwa sasa ambao umeonekana kukua mara tatu zaidi ndani ya miaka mitano iliyopita.

Dk. Kaushik alisema kuwa, mbali na mjadala wa uchunguzi wa kisayansi, Mambo mengine yatakayo jadiliwa ni pamoja na

• Kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari katika nchi zinazoendelea, na lengo hasa juu Africa na namna ya kutatua matatizo yatokanayo.
• Kujadili kuhusu mzigo wa kijamii na kiuchumi unaotokana na watu wenye ugonjwa wa kisukari , familia zao na jamii kwa ujumla.
• Umuhimu wa kutafuta ufumbuzi wa Ugonjwa huu.
• Taarifa za uchunguzi za wataalam ngazi za mkoa.

Post a Comment