10
Nov

MATEMBEZI KWA AJILI YA KUJENGA UFAHAMU JUU YA UWEPO WA WATOTO WENYE UGONJWA WA KISUKARI TANZANIA.

393713_317636731588734_544903010_nKisukari ni ugonjwa ambao unakuwa kwa kasi sana Duniani. Kisukari ni mojawapo ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na huchangia asilimia mbili (2%) ya vifo vinavyosababishwa na magojwa hayo. Kisukari kinakadiriwa kusababisha vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoyakuambukiza kwa asilimia saba (7%) kufikia mwaka 2030. Kila mwaka Taasisi ya WORLD DIABETES FOUNDATION inaandaa matembezi yaitwayo Global Diabetes Walk kila tarehe 14 ya mwezi November. Dhumuni la matembezi haya ni kuwaamsha watu katika kupambana na ugonjwa huu hatari Duniani.

 

TANZANIA DIABETES ASSOCIATION –TDA (Chama cha Ugonjwa wa Kisukari) kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wameandaa matembezi kwa ajili ya kujenga ufahamu juu ya uwepo wa watoto wenye kisukari Tanzania ambayo yatafanyika tarehe 12 November 2016 siku ya Jumamosi (kwa sababu siku ya 14 November 2016 ni siku ya Jumatatu ambayo ni siku ya kazi). Watoto wenye Kisukari mia moja (100) watatembea kwa pamoja kuiadhimisha siku ya kisukari Duniani. Idadi ya washiriki wote haitazidi watu 250.

 

Mkiwa kama wadau muhimu tunapenda  kuwakaribisha kushiriki.

  • Muda wa Kuanza matembezi: 12.30 asubuhi
  • Muda wa kumaliza: 00 Mchana.
  • Mgeni Rasmi wa tukio hili atakuwa Mama Salma Kikwete.

 

Mkusanyiko utakuwa Fukwe za agakhan.

Matembezi yataanzia Fukwe za agakhan, kupitia barabara ya Barack Obama, barabara ya Umoja wa Mataifa, na kumalizikia Muhimbili.

Baada ya Matembezi haya, Mgeni Rasmi atapata Fursa ya kuongea na Watoto wenye kisukari Tanzania na kuongea na vyombo vya habari juu ya changamoto zinazowapata watoto wenye Kisukari Tanzania na namna ya kuzitatua.

 

Matembezi haya yanalenga kuondoa unyanyapaa kwa watoto wenye kisukari Tanzania na kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi kama ni moja ya njia kuu ya kupambana na magonjwa yasio ambukiza. Kisukari  ni mojawapo ya magonjwa hayo.

 

Kauli mbiu ya matembezi haya ni “EYES ON DIABETES” na “Test2Prevent”. KUWA MAKINI NA KISUKARI na PIMA KUJIKINGA.

Post a Comment